Yesu mbele ya baraza la wazee
53 Nao wakamchukua Yesu kwa Kuhani Mkuu; wakamkusanyikia wote, wakuu wa makuhani na wazee na waandishi. 55 Mt 26:59-68;Lk 22:63-71;Yn 18:19-24Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda juu ya Yesu wapate kumwua; wasione. 61 Mk 15:5;Isa 53:7Lakini akanyamaza, wala hakujibu neno. Kuhani Mkuu akamwuliza tena, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mtukufu? 62 Dan 7:13;Zab 110:1Yesu akasema, Mimi ndiye, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kulia wa nguvu, akija na mawingu ya mbinguni. 63 Kuhani Mkuu akararua nguo zake, akisema, Tuna haja gani tena ya mashahidi? 64 Law 24:16;Yn 19:7Mmesikia kufuru yake; mwaonaje ninyi? Wote wakamhukumu kuwa imempasa kuuawa.