Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 15:21,22,24-27

SRUV Swahili Revised Union Version

Kusulubiwa kwa Yesu

21 Rum 16:13Wakamshurutisha mtu aliyekuwa akipita, akitoka mashambani, Simoni Mkirene, baba yao Iskanda na Rufo, ili auchukue msalaba wake. 22 Wakamleta mpaka mahali paitwapo Golgotha, yaani, Fuvu la kichwa. 24 Zab 22:18Wakamsulubisha, wakagawa mavazi yake, wakayapigia kura kila mtu atwae nini. 25 Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulubisha. 26 Palikuwa na anwani ya mashitaka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI. 27 Na pamoja naye walisulubisha wanyang’anyi wawili, mmoja mkono wake wa kulia na mmoja mkono wake wa kushoto. [

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    21 Mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, baba yao Iskanda na Rufo, alikuwa anaingia mjini kutoka mashambani, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba. 22 Kisha wakampeleka Isa hadi mahali palipoitwa Golgotha (maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa). 24 Basi wakamsulubisha, nazo nguo zake wakagawana miongoni mwao kwa kuzipigia kura ili kuamua ni gani kila mtu ataichukua.

    25 Ilikuwa saa tatu asubuhi walipomsulubisha. 26 Tangazo likaandikwa la mashtaka dhidi yake lenye maneno haya:

    Mfalme wa Wayahudi.

    27 Pamoja naye walisulubiwa wanyang’anyi wawili, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wa kushoto. [

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    21 Mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, baba yao Aleksanda na Rufo, alikuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shamba, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba. 22 Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgotha (maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa). 24 Basi wakamsulubisha, nazo nguo zake wakagawana miongoni mwao kwa kuzipigia kura ili kuamua ni gani kila mtu ataichukua.

    25 Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha. 26 Tangazo likaandikwa la mashtaka dhidi yake lenye maneno haya: "Mfalme wa Wayahudi." 27 Pamoja naye walisulubiwa wanyangʼanyi wawili, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wa kushoto. [

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.