Pular para o conteúdo
Publicidade

Marcos 3

22 Mt 12:24-32;Lk 11:15-22;12:10Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, Ana Beelzebuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo.Mt 9:34;10:2523 Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani? 24 Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama; 25 na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama. 26 Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake, akafitinika, hawezi kusimama, bali huwa na kikomo. 27 Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake. 28 Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; 29 Lk 12:10bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele, 30 Mk 3:22kwa vile walivyosema, Ana pepo mchafu.

Veja também