Jamaa wa kweli wa Yesu
31 Mt 12:46-50;Lk 8:19-21Wakaja mamaye na nduguze; wakasimama nje, wakatuma mtu kumwita. 32 Na makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka, wakamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta. 33 Akawajibu, akisema, Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani? 34 Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akasema, Tazama, mama yangu na ndugu zangu! 35 Kwa maana mtu yeyote atakayeyafanya mapenzi ya Mungu, huyo ndiye kaka yangu, na dada yangu, na mama yangu.