Pular para o conteúdo
Publicidade

Marko 4:26-29

SRUV Swahili Revised Union Version

Mfano wa mbegu inayokua

26 Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi; 27 Yak 5:7akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye. 28 Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke. 29 Yoe 3:13Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    26 Pia akawaambia, "Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. 27 Baada yake kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo. 28 Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke. 29 Mara nafaka inapokuwa imekomaa, mkulima huenda shambani na mundu kuvuna, maana mavuno yamekuwa tayari."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    26 Pia akawaambia, "Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. 27 Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo. 28 Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke. 29 Lakini nafaka inapokuwa imekomaa, mara mkulima huingia shambani na mundu wa kuvunia, maana mavuno yamekuwa tayari."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.