11 Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu chochote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi; 12 wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye; 13 huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokezana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo. 14 Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu. 15 Mdo 10:14,15Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu. [