Yesu amponya mtu aliyekuwa kiziwi
31 Mt 15:29-31Akatoka tena katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka ziwa la Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli. 32 Mk 5:23Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono. 33 Mk 8:23Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, 34 Mk 6:41;Yn 11:41akatazama juu mbinguni, akapiga kite, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. 35 Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri. 36 Mk 1:43-45Akawaonya wasimwambie mtu; lakini kadiri ya alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari; 37 Isa 35:5wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, Ametenda mambo yote vema; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme.