1 Kwa maana,4:1 Kwa maana, Sura ya 4:1-6 ni Sura 3:19-24 katika Kiebrania. angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi. 2 Lk 1:78;Efe 5:14;2 Pet 1:19 Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawachomozea, likiwa na uwezo wa kuponya katika miale yake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama watokapo mazizini. 3 Mik 7:10 Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi.
4 Kum 4:10 Ikumbukeni Torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu. 5 Yoe 2:31;Mt 11:14;17:10-13;Mk 9:11-13;Lk 1:17;Yn 1:21 Angalieni, nitawatumia Eliya nabii, kabla siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya haijafika. 6 Lk 1:17;Dan 9:26;Lk 19:27,43;21:20;Mk 13:14 Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.