Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 1

Ukoo wa Yesu Kristo

1 Lk 3:23-381 Nya 17:11;Mwa 5:1;22:18Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu.

2 Mwa 21:3,12;25:26;29:35;49:10;1 Nya 1:34Abrahamu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; 3 1 Nya 2:5,9;Mwa 38:29,30;Rut 4:18-22;1 Nya 2:10-12Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu; 4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni; 5 Rut 4:13-17Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese; 6 2 Sam 12:24Yese akamzaa mfalme Daudi.

Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria; 7 1 Nya 3:10-14Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa; 8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia; 9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia; 10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia; 11 2 Fal 24:14-15;2 Nya 36:10;Yer 27:20;1 Nya 3:15,16Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.

12 1 Nya 3:17;Ezr 3:2Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli; 13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori; 14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi; 15 Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo; 16 Mt 27:17,22Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.

17 Basi vizazi vyote tangu Abrahamu hadi Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hadi ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hadi Kristo ni vizazi kumi na vinne.

Veja também