37 Kum 33:9;Lk 14:26,27Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. 38 Mt 16:24;Mk 8:34;Lk 9:23Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. 39 Mt 16:25;Mk 8:35;Lk 9:24;17:33;Yn 12:25Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.