1 Mk 6:7-13;Lk 9:1-5 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
2 Mk 3:14-19;Lk 6:13-16;Yn 1:40-49 Na majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya; Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye; 3 Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Thadayo; 4 Simoni Mkananayo, na Yuda Iskarioti, naye ndiye aliyemsaliti.
5 Hao Kumi na Wawili Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie. 6 Mt 15:24;Mdo 13:46;Yer 50:6 Bali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 7 Lk 10:4-12 Na katika kuenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.Mt 4:17;Lk 10:98 Mdo 20:33 Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. 9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala pesa mishipini mwenu; 10 1 Kor 9:14;1 Tim 5:18;Lk 10:4;Hes 18:31 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mfanyakazi astahili posho yake. 11 Na mji wowote au kijiji chochote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hadi mtakapotoka. 12 Lk 10:5,6 Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni. 13 Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi. 14 Mdo 13:51;18:6;Lk 10:10-12 Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu. 15 Mt 11:24;Mwa 19:24-28;Lk 20:47 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule.
16 Lk 10:3;Yn 10:12;Mdo 20:29;Rum 16:19;Efe 5:15 Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua. 17 Mk 13:9-11;Lk 12:11-12;21:12-15 Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;Mt 24:918 Mt 24:14;Mdo 25:23;27:24 nanyi mtachukuliwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa. 19 Lk 12:11,12 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikirifikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. 20 Yn 14:26;1 Kor 2:4 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu. 21 Mk 13:12;Lk 21:16;Mt 10:35;Mik 7:6 Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwaua. 22 Mt 24:9,13;Mk 13:13;Lk 21:17;Yn 15:21 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. 23 Mt 16:28 Lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.
24 Lk 6:40;Yn 13:16;15:20 Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake. 25 Mt 9:34;12:24;Mk 3:22;Lk 11:15 Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?
26 Lk 12:2-9 Basi, msiwaogope, kwa maana hakuna neno lililositirika, ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa, ambalo halitajulikana.Mk 4:22;Lk 8:1727 Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba. 28 Yak 4:12 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanamu.
29 Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu; 30 lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. 31 Mt 12:12 Msiogope basi; bora ninyi kuliko mashomoro wengi. 32 Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. 33 2 Tim 2:12;Lk 9:26 Bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
34 Lk 12:51-53 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga. 35 Mik 7:6 Kwa maana nilikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; 36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake. 37 Kum 33:9;Lk 14:26,27 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. 38 Mt 16:24;Mk 8:34;Lk 9:23 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. 39 Mt 16:25;Mk 8:35;Lk 9:24;17:33;Yn 12:25 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.
40 Mk 9:37;Lk 9:48;10:16;Yn 12:44;13:20;Mt 18:5 Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. 41 Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki. 42 Mt 25:40;Mk 9:41 Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa angaa kikombe cha maji baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake.