Publicidade

Mateus 13

Yesu aelezea mfano wa magugu

36 Mt 13:24-30Kisha Yesu akawaaga makutano, akaingia katika nyumba; wanafunzi wake wakamwendea, wakasema, Tufafanulie mfano wa magugu ya shambani. 37 Akajibu, akasema, Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu; 38 1 Kor 3:9lile shamba ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu; 39 yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika. 40 Yn 15:6Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia. 41 Sef 1:3;Mt 25:31-46;7:23Mwana wa Adamu atawatuma malaika wake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, 42 Mt 8:12na kuwatupa katika tanuri ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. 43 Dan 12:3Ndipo wenye haki watakapong’aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-