Petro amkiri Yesu kuwa Kristo
13 Mk 8:27-30;Lk 9:18-21Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? 14 Mt 14:1-2;17:10;Mk 6:14-15;Lk 9:7-8Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. 15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16 Yn 6:68-69Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.