Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 17

Kugeuka sura

1 2 Pet 1:17-18Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani; 2 2 Pet 1:16-18akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru. 3 Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye. 4 Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. 5 Mwa 22:2;Kum 18:15;Zab 2:7;Isa 42:1;Mt 3:17;12:18;Mk 1:11;Lk 3:22Alipokuwa bado akisema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.

Veja também