Yesu aponya mvulana mwenye pepo
14 Mk 9:14-29;Lk 9:37-42Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema, 15 Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. 16 Nilimleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya. 17 Kum 32:5;Yn 14:9Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hadi lini? Nitachukuliana nanyi hadi lini? Mleteni huku kwangu. 18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule mvulana akapona tangu saa ile.