Yesu na ushuru wa hekalu
24 Kut 30:13;38:26Na walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi ushuru wa hekalu?17:24 yaani nusu shekeli. Akasema, Hutoa. 25 Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni? 26 Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana wako huru. 27 Lakini tusije tukawakwaza, nenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli;17:27 Shekeli moja ni kama shilingi 3. ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.