Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 18

Kusameheana

21 Lk 17:3-4Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? 22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.

Mfano wa mtumishi asiyesamehe

23 Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. 24 Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja mwenye deni la talanta18:24 Talanta moja ni kama shilingi 5,000. elfu kumi. 25 Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, ikalipwe ile deni. 26 Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. 27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. 28 Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa watumishi wake, aliyemwia dinari18:28 Dinari moja ni kama senti 75. mia; akamkamata, akamkaba koo, akisema, Nilipe unachodaiwa. 29 Basi mtumwa mwenzake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. 30 Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa gerezani, hadi atakapoilipa ile deni. 31 Basi watumwa wenzake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. 32 Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nilikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; 33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mtumwa mwenzako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? 34 Mt 5:26Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. 35 Mt 6:14,15Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.

Veja também