3 Mk 10:15;Lk 18:17;Mt 19:14;Yn 3:3-5akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama watoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Majaribu ya dhambi
4 Basi, yeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. 5 Mt 10:40;Yn 13:20Na yeyote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi;