Mauaji ya watoto wachanga
16 Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale majusi, alighadhibika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wa kiume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake kote, kuanzia wenye miaka miwili na chini yake, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale majusi. 17 Yer 31:15Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema,
18 Yer 31:15;Mwa 35:19Sauti ilisikiwa Rama,
Kilio na maombolezo mengi,
Raheli akiwalilia watoto wake,
Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawapo tena.