Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 2

3 Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. 4 Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? 5 Mik 5:2;Yn 7:42Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Yudea; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,

6 Mik 5:1Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,

Hu mdogo kamwe miongoni mwa watawala wa Yuda;

Kwa kuwa kwako atatoka mtawala

Atakayewachunga watu wangu Israeli.

7 Kisha Herode akawaita wale majusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota. 8 Akawatuma Bethlehemu, akasema, Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.

Veja também