26 Mt 23:11;Mk 9:35;Lk 22:26Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; 27 na mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; 28 Lk 22:27;Flp 2:7;1 Tim 2:6kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.