Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 21

Yesu Aulaani Mtini

18 Na asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. 19 Lk 13:6Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara. 20 Wanafunzi walipoona, walistaajabu, wakisema, Jinsi gani mtini umenyauka mara? 21 Mt 17:20;1 Kor 13:2Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka. 22 Na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.

Veja também