Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 22

Swali kuhusu ufufuo

23 Mk 12:18-27;Lk 20:27-40Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,Mdo 23:824 Kum 25:5,6;Mwa 38:8wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao. 25 Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake. 26 Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba. 27 Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. 28 Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi kati ya wale saba? Maana wote walikuwa naye. 29 Yesu akajibu, akawaambia, Mnapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu. 30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni. 31 Tena kuhusu kiyama ya wafu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema, 32 Kut 3:6;Mt 8:11Mimi ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. 33 Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake.

Veja também