Kuja kwa Mwana wa Adamu
29 Isa 13:10;34:4;Eze 32:7;Yoe 2:10;3:4;3:15;Ufu 6:12-13;2 Pet 3:10Lakini mara tu, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka kutoka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 Dan 7:13;Zek 12:10-14;Ufu 1:7;19:11;Mt 26:64ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.