Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 25

Mfano wa wanawali kumi

1 Lk 12:35;Ufu 19:7Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. 3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; 4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. 5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. 6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. 7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. 8 Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. 9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. 10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. 11 Lk 13:25Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. 12 Mt 7:23Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. 13 Mt 24:42Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.

Veja também