Mpango wa kumwua Yesu
1 Mt 7:28;11:1;13:53;19:1Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake, 2 Mk 14:1,2;Lk 22:1,2Mnajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa asulubiwe.Kut 12:1-27;Mt 20:183 Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa; 4 wakafanya shauri pamoja, ili wamkamate Yesu kwa hila na kumwua. 5 Lakini wakasema, Isiwe wakati wa sikukuu, isije ikatokea ghasia miongoni mwa watu.
Yesu apakwa mafuta Bethania
6 Mk 14:3-9;Lk 7:36-50;Yn 12:1-8Naye Yesu alipokuwapo Bethania katika nyumba ya Simoni mwenye ukoma, 7 Lk 7:37-38mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya thamani kubwa alimkaribia akaimimina kichwani pake alipoketi chakulani. 8 Wanafunzi wake walipoona, wakakasirika, wakasema, Ni wa nini upotevu huu? 9 Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa fedha nyingi wakapewa maskini. 10 Lk 11:7Yesu akatambua akawaambia, Mbona mnamtaabisha mwanamke? Maana ni kazi njema aliyonitendea mimi. 11 Kum 15:11Kwa maana siku zote mnao maskini pamoja nanyi; lakini mimi hamko nami siku zote. 12 Maana kwa kunimwagia mwili wangu marhamu hiyo, ametenda hivyo ili kuniweka tayari kwa maziko yangu. 13 Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu yake.
Yuda akubali kumsaliti Yesu
14 Mk 14:10,11;Lk 22:3-6Wakati huo mmoja wa wale Kumi na Wawili, jina lake Yuda Iskarioti, aliwaendea wakuu wa makuhani, 15 Zek 11:12;Yn 11:57akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.26:15 Yapata kama shilingi 90.16 1 Tim 6:9,10Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi apate kumsaliti.
Yesu katika Pasaka pamoja na wanafunzi
17 Mk 14:12-16;Lk 22:7-13Katika siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Ni wapi utakapo tukuandalie uile Pasaka?Kut 12:18-2018 Mt 21:3Akasema, Nendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu asema, Majira yangu ni karibu; kwako nitafanya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu. 19 Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaagiza, wakaiandaa Pasaka. 20 Mk 14:17-26;Lk 22:14-23;Yn 13:21-26Basi kulipokuwa jioni aliketi chakulani pamoja na wale Kumi na Wawili. 21 Nao walipokuwa wakila, alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu atanisaliti. 22 Wakahuzunika sana, wakaanza kumwuliza mmoja mmoja, Ni mimi, Bwana? 23 Zab 41:10Akajibu akasema, Yeye aliyetia mkono wake pamoja nami katika bakuli, ndiye atakayenisaliti. 24 Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa. 25 Yuda, yule mwenye kumsaliti, akajibu, akasema, Ni mimi, Rabi? Akamwambia, Wewe umesema.
Kuanzishwa kwa chakula cha Bwana
26 Mt 14:19;1 Kor 11:23-25Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu 27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Kuyweni nyote katika hiki; 28 Kut 24:8;Yer 31:31-34;Zek 9:11kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.