Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 27

Yuda ajinyonga

3 Mdo 1:18-19;Mt 26:15Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nilikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia. 4 Wakasema, Basi, haya yatuhusu nini sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe. 5 Mdo 1:18;2 Sam 17:23Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.

Veja também