Kufufuka kwa Yesu
1 Mk 16:1-10;Lk 24:1-10;Yn 20:1-18Na sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. 5 Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. 6 Mt 12:40;16:21;17:23;20:19;Mdo 2:36Hayupo hapa; maana amefufuka kama alivyosema. Njooni, mpatazame mahali alipolazwa. 7 Mt 26:32Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia.