2 Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia. 4 Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu. 6 Mt 12:40;16:21;17:23;20:19;Mdo 2:36Hayupo hapa; maana amefufuka kama alivyosema. Njooni, mpatazame mahali alipolazwa.
Ripoti ya walinzi
11 Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya walinzi waliingia mjini, wakawaambia wakuu wa makuhani juu ya mambo yote yaliyotendeka. 12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, 13 Mt 27:64wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala.