Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 3

Mahubiri ya Yohana Mbatizaji

1 Mk 1:1-8;Lk 3:3-18Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Yudea, na kusema,Lk 1:132 Mt 4:17;Mk 1:15Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. 3 Isa 40:3;Yn 1:23Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema,

Sauti ya mtu aliaye nyikani,

Itengenezeni njia ya Bwana,

Yanyosheni mapito yake.

4 2 Fal 1:8Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.

5 Ndipo walipomwendea wa Yerusalemu, na wa Yudea wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; 6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.

Veja também