Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 4

Majaribu ya Yesu

1 Mk 1:12,13;Lk 4:1-13Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.Ebr 2:18;4:152 Kut 34:28;1 Fal 19:8Akafunga siku arubaini mchana na usiku, mwishowe akaona njaa. 3 Mwa 3:1-7Mjaribu akamjia akamwambia, Ikiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate. 4 Kum 8:3Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. 5 Mt 27:53Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, 6 Zab 91:11-12akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana imeandikwa,

Atakuagizia malaika zake;

Na mikononi mwao watakuchukua;

Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

7 Kum 6:16Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. 8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka katika mlima mrefu mno, akamwonesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, 9 akamwambia, Haya yote nitakupa, ukiinama na kunisujudia. 10 Kum 6:13Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake. 11 Yn 1:51;Ebr 1:6,14Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.

Veja também