Kuhusu hasira
21 Kut 20:13;21:12;Law 24:17;Kum 5:17;17:8Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. 22 1 Yoh 3:15Bali mimi nawaambieni, Kila amkasirikiaye ndugu yake itampasa hukumu; na mtu akimtusi ndugu yake, anastahili kuhukumiwa na baraza; na mtu akimwambia nduguye, Ewe mpumbavu, anastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
Kuhusu uzinzi
27 Kut 20:14;Kum 5:18Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28 Ayu 31:1;2 Pet 2:14lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.