Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 5

Upendo kwa adui

43 Law 19:18Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; 44 Kut 23:4,5;Rum 12:14,20;Lk 23:34;Mdo 7:59lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, 45 Efe 5:1ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mnapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? 47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi sawa na hayo? 48 Law 19:2;Kum 18:13Basi ninyi iweni wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Veja também