Msisumbuke
25 Lk 12:22-31Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?Flp 4:6;1 Pet 5:7;1 Tim 6:6;Ebr 13:5
26 Mt 10:29-31Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao? 31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Mt 6:8Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Rum 14:17;1 Fal 3:13,14;Zab 37:4,25Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34 Kut 16:19Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Maovu ya siku yanaitosha siku hiyo.