9 Lk 11:2-4;Yn 17:6Basi ninyi salini hivi;
Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
10 Mt 7:21;Lk 22:42Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Mt 14:15;18:21-35Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 1 Nya 29:11-13;Yn 17:11,15Na usitutie majaribuni,
lakini utuokoe na yule mwovu.
[Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.
Amina.]