Mlango mwembamba
13 Lk 13:24;Yn 10:7,9Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. 14 Mt 19:24;Mdo 14:22Bali mlango ni mwembamba, na njia imebana iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.