Mti na matunda yake
15 Mt 24:4,5,24;Mdo 20:29Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali. 16 Gal 5:19-22;Yak 3:12Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17 Mt 12:33Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. 18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. 19 Mt 3:10;Lk 3:9;Yn 15:2,6Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 20 Mt 12:33Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.