Yesu atuliza dhoruba
23 Mk 4:36-41;Lk 8:23-25Akapanda katika mashua, wanafunzi wake wakamfuata.Zab 4:824 Kukawa na msukosuko mkuu baharini, hata mashua ikafunikwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi. 25 Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia. 26 Mt 14:31;16:8Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu. 27 Wale watu wakamaka wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani hata pepo na bahari zamtii?