Yesu amponya mtumishi wa afisa
5 Lk 7:1-10Na alipoingia Kapernaumu, afisa mmoja alimjia,Yn 4:476 akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. 7 Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye. 8 Yule afisa akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. 9 Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya. 10 Mt 15:28Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa yeyote katika Israeli. 11 Lk 13:29;Isa 49:12;59:19;Mal 1:11;Zab 107:3Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; 12 Mt 22:13;24:51;25:30;Lk 13:28bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. 13 Mt 9:29;15:28Naye Yesu akamwambia yule afisa, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona wakati ule ule.