Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 9

Yesu awaponya vipofu wawili

27 Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Mwana wa Daudi. 28 Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana. 29 Mt 8:13Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu na itendeke kwenu. 30 Mt 8:4Macho yao yakafumbuka. Naye Yesu akawaagiza kwa nguvu, akisema, Angalieni hata mtu mmoja asijue. 31 Lakini wakatoka, wakaeneza habari zake katika nchi ile yote.

Veja também