Utaratibu wa kazi
1 Neh 12:10,39;Yn 5:2;Yer 31:38;Zek 14:10Ndipo akaondoka Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na nduguze makuhani, wakalijenga lango la kondoo; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake; mpaka mnara wa Hamea wakalitakasa, mpaka mnara wa Hananeli. 12 Kut 35:25;Lk 8:3;Flp 4:3Na baada yake akajenga Shalumu, mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu ya sehemu ya Yerusalemu,3:12 Tazama 3:9. yeye na binti zake. 28 2 Fal 11:16;2 Nya 23:15;Yer 31:40Juu ya lango la farasi wakajenga makuhani, kila mtu kuielekea nyumba yake. Baada yao akajenga Sadoki, mwana wa Imeri, kuielekea nyumba yake.