Ukarimu wa Nehemia
14 Neh 13:6;1 Kor 9:4Tena tangu wakati huo nilipowekwa kuwa mtawala wao katika nchi ya Yuda, tangu mwaka wa ishirini hadi mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta mfalme, yaani, miaka kumi na miwili, mimi na ndugu zangu hatukula chakula cha mtawala. 15 2 Kor 11:9;Mwa 42:18;Ayu 31:23;Zab 112:1;Mit 16:6;Mhu 12:13,14;Lk 18:2-4Lakini watawala wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arubaini za fedha; tena hata watumishi wao nao wakawatawala watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nilimcha Mungu. 16 Naam, hata kazi ya ukuta huu tena nikaishika sana, wala hatukujipatia mashamba; na watumishi wangu wote wakakusanyika huko kazini. 17 2 Sam 9:7Pamoja na hayo wakawako mezani pangu, katika Wayahudi na maofisa, watu mia moja na hamsini, zaidi ya wale waliotujia kutoka kwa mataifa yaliotuzunguka. 18 1 Fal 4:22Basi, maandalizi ya chakula yaliyoandaliwa kila siku yalikuwa ng’ombe mmoja na kondoo sita wazuri; tena nikaandaliwa kuku, na mara moja katika siku kumi akiba ya mvinyo ya namna zote; wala kwa hayo yote sikudai marupurupu ya chakula cha mtawala, kwa kuwa watu walikuwa wamebeba mzito mzito. 19 Neh 13:22Unikumbuke, Ee Mungu wangu, kwa mema, wote niliowatendea watu hawa.