12 Mdo 10:34;15:9Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Mgiriki; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye ukarimu10:12 Au ‘mwenye utajiri’. mwingi kwa wote wamwitao; 13 Yoe 2:32kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. 14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? 15 Isa 52:7Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
16 Isa 43:1Lakini si wote walioitii ile Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeziamini habari zetu? 17 Yn 17:20Basi imani, hutokana na kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.