Publicidade

Romanos 12

Maisha mapya katika Kristo

1 Rum 6:11,13;1 Pet 2:5;Yn 4:24 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. 2 Efe 4:23;5:10,17;Rum 1:28;Gal 1:4 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

3 1 Kor 12:11;Efe 4:7 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinuie makuu kupita ilivyompasa kunuia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. 4 1 Kor 12:12 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; 5 1 Kor 12:27;Efe 4:25 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. 6 1 Kor 12:4-11 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa ni unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; 7 1 Pet 4:10,11 ikiwa ni huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; 8 Mt 6:3;2 Kor 8:2;9:7 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; msimamizi, na asimamie kwa bidii; anayerehemu, na arehemu kwa furaha.

Sifa za Mkristo

9 1 Pet 1:22;1 Tim 1:5;Amo 5:15 Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkilishika lililo jema. 10 2 Pet 1:7;Flp 2:3 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; 11 Ufu 3:15;Mdo 18:25 kwa bidii, bila kulegea; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; 12 1 The 5:17 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; mkidumu katika kusali; 13 Ebr 13:2 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi. 14 Mt 5:44;Lk 6:28;Mdo 7:59;1 Kor 4:12 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. 15 Zab 35:13 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. 16 Mit 3:7;Rum 15:5;11:20 Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinuie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili. 17 Isa 5:21;1 The 5:15 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 Mk 9:50;Ebr 12:14 Ikiwezekana, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. 19 Kum 32:35;Law 19:18;Mt 5:39;2 The 1:6,7;Rum 13:4;Ebr 10:30 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. 20 Mit 25:21-22;Mt 5:44 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. 21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-04_23-13-58-