Pular para o conteúdo
Publicidade

Warumi 12:17-21

SRUV Swahili Revised Union Version

17 Isa 5:21;1 The 5:15Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 Mk 9:50;Ebr 12:14Ikiwezekana, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. 19 Kum 32:35;Law 19:18;Mt 5:39;2 The 1:6,7;Rum 13:4;Ebr 10:30Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. 20 Mit 25:21-22;Mt 5:44Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. 21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    17 Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 Ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote. 19 Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: "Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza," asema Mwenyezi Mungu. 20 Badala yake:

    "Kama adui yako ana njaa, mlishe;

    kama ana kiu, mpe kinywaji.

    Kwa kufanya hivyo,

    unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake."

    21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    17 Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 Kama ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote. 19 Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: "Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza," asema Bwana. 20 Badala yake:

    "Kama adui yako ana njaa, mlishe;

    kama ana kiu, mpe kinywaji.

    Kwa kufanya hivyo,

    unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake."

    21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.