Usimhukumu mwingine
1 Kol 2:16;Rum 15:1;1 Kor 8:9Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, lakini msimhukumu mawazo yake. 2 Mwa 1:29;9:3Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga. 3 Kol 2:16Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali. 4 Mt 7:1;Yak 4:11,12Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.