Hukumu ya Mungu yenye haki
1 Mt 7:1;Lk 6:37;Yn 8:7Kwa hiyo, wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru; kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale. 2 Nasi tunajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. 3 Wewe binadamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! Wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu?