6 Zab 62:12;Mit 24:12;Mt 16:27;Yn 5:29;2 Kor 5:10atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; 7 wale ambao kwa subira katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoharibika, watapewa uzima wa milele; 8 2 The 1:8na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu; 9 Rum 1:16;3:9dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Mgiriki pia; 10 bali utukufu na heshima na amani kwa kila mtu atendaye mema, Myahudi kwanza na Mgiriki pia; 11 Kum 10:17;Mdo 10:34;1 Pet 1:17kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.