Haki kupitia kwa imani
21 Mdo 10:43;Rum 1:17Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na Torati na Manabii; 22 Gal 2:16ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; 23 Rum 9:19;5:2kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24 Rum 5:1;Efe 2:8wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; 25 Law 16:12-15;Ebr 4:16;Efe 1:7ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho3:25 Upatanisho hapa maana yake ni, Kiti cha rehema. kwa njia ya imani katika damu yake, ili aoneshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; 26 apate kuonesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yeye amwaminiye Yesu.