Matokeo ya kuhesabiwa haki
1 Rum 3:24,28;4:24;Isa 53:5Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na muwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, 2 Efe 3:12;Rum 3:23ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. 3 Yak 1:2,3;1 Pet 1:5-7Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta subira; 4 na kazi ya subira ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; 5 Zab 22:5;25:20;Ebr 6:18,19na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.